Virusi vya corona: 'Mabadiliko ya utaratibu wa Hija yametufanya tulie'

Maelezo ya video, Virusi vya corona: 'Mabadiliko ya utaratibu wa Hija yamtufanya tulie'

Shadia anaongoza jopo linalofanya kazi ya kuwaongoza wanawake wazee kwenye shughuli za Hija katika mji Mtakatifu wa Mecca.

Lakini kuna jambo moja ambalo hufanya jopo lake kuwa la kipekee- ni magari ya kijani ya kielektroniki ambayo huyatumia kuzunguka mjini.

Lakini janga la virusi vya corona limefanya kazi yao kuwa ngumu sana, kutokana na hatua zinazochukuliwa kudhibiti maambukizi.