Je uhusiano wa karibu kati ya Uingereza na Hongkong utaathiri ule wa China?
Jifahamishe kuhusu historia ya mahusiano kati ya pande hizo mbili na kwanini hofu iliopo inaweza kubadilisha uhusiano uliopo kati ya China na Uingereza kabisa.
China hivi majuzi iliiwekea Hongkong sheria ya usalama ilio na utata , ikitoa adhabu kali dhidi ya uhalifu.
Hatua hiyo imewawacha wakaazi wa eneo hilo kuwa na wasiwasi kwamba uhuru wao utapotea na kwamba mfumo wao wa maisha utakuwa sawa na ule wa China bara.