Upasuaji huo wa kipekee ulichukua takriban saa 18
Baada ya saa 18 ya upasuaji hatari, madaktari katika hospitali ya Bambino Gesu mjini Rome Italia, wamefanikiwa kuwatenganisha mapacha waliokuwa wameshikamana. Ervina na Prefina, kutoka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, walikuwa wameshikamana upande wa nyuma wa kichwa tangu walipozaliwa