‘Ninataka wasichana wawe madaktari au waalimu’: Ndoto ya mkulima wa Muafghanstan
Wasichana wa Afghanstan ambao hawasomi, wanakabiliwa na hatari mara tatu ya kuingia katika ndoa za utotoni kuliko wasichana waliosoma hadi shule za sekondari, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shilika la haki za binadamu la Human Rights Watch. Zaidi ya watoto milioni 3.7 wamenyimwa haki ya elimu nchini Afghanistan. Wengi wao ni wasichana. Lakini mwanaume mmoja amekuja na wazo la kukabiliana na changamoto hii katika kijiji chake.