Virusi vya corona: Fahamu jinsi Sierra Leone inavyodhibiti maambukizi

Maelezo ya video, Jinsi Sierra Leone inavyokabiliana na corona

Sierra Leone ilikuwa ni moja ya nchi za Afrika Magharibi iliyoathirika zaidi na janga la Ebola, 2014. Na sasa hivi inakabiliana na ugonjwa wa virusi vya corona.

Mtu wa kwanza kuthibitishwa kuwa na corona Machi 31 na tangu wakati huo idadi ya wanaopata maambukizi imekuwa ikiongezeka.

Tyson Conteh ni mtengenezaji filamu huko Makeni, mji wa kaskazini mwa Sierra Leone.

Alifuatilia mlipuko wa Ebola kupitia BBC Africa Eye na sasa hivi ametengeneza mfululizo wa video kufuatilia vile mji huo unavyokabiliana na virusi vya corona katika makala ya BBC Africa Eye.

Katika mfululizo wa tano wa video hizo, anaangazia vile Sierra Leone inavyotumia tena mfumo wa kufuatilia watu kukabiliana na virusi vya corona.

Mfumo huo ulikuwa muhimu sana katika kukabilina na janga la Ebola ambalo lilikumba nchi hiyo 2014. Lakini licha ya tajriba iliyopita, Sierra Leone imekuwa na changamoto katika utumiaji wa mfumo huohuo kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.