Maandamano ya George Floyd yasambaa hadi Uarabuni
Kifo cha George Floyd nchini Marekani kimetoa msukumo kwa Waarabu weusi kuandamana katika mataifa yao dhidi ya ubaguzi wa rangi na unyanyapaa. Wakosoaji nchini Tunisia wamesema ubaguzi wa rangi umeendelea kupuuzwa.