Domitien Ndayizeye aliyekuwa rais wa Burundi asikitishwa na kifo cha Pierre Nkurunziza
Domitien Ndayizeye aliyekuwa rais wa Burundi kuanzia mwaka 2003 hadi 2005 amezungumzia kusikitishwa kwake na taarifa za kifo cha rais Pierre Nkurunziza.
Bwana Ndayizeye alimrithi Pierre Buyoya kama rais April 30, 2003 baada ya kuwa naibu wa rais Buyoya kwa miezi 18. Ndayizeye alisalia madarakani hadi aliporithiwa na Pierre Nkurunziza Agosti 26, 2005.
Domitien Ndayizeye amezungumzia mfumo ulio wazi na kwa sasa hivi kilichopo ni kusibiri tu hatua itakayochukuliwa na serikali baada ya kifo cha rais Pierre Nkurunziza kuonesha njia ya kufuatwa.
Sikiliza mahojiano yake na mwanahabri wa BBC Roncliff Odit.
