Wakimbizi wa Rohingya 'walazimika kunywa maji ya bahari kuokoa maisha' baada ya kufurushwa

Maelezo ya video, Wakimbizi wa Rohingya 'walazimika kunywa maji ya bahari kuokoa maisha' baada ya kufurushwa

Taifa la Malaysia lililifurusha boti lililokuwa limebeba mamia ya wakimbizi wa Rohingya , likihofia maambukizi ya virusi vya corona .

Kufikia muda ambapo boti hilo liliokolewa na walinzi wa pwani ya Bangladesh , kati ya wakimbizi 20 hadi 50 walikuwa wamefariki.

Na bado wengine wanaaminika kukwama baharini wakitafuta bandari ilio salama