Tunaangazia maisha ya mtoto katika mgodi nchini Ghana

Maelezo ya video, Watoto wanaotafuta madini migodini nchini Ghana

Licha ya kwamba Ghana ina migodi mingi ya dhahabu, maelfu ya wachimbaji wanafanyakazi hiyo kiharamu lakini wana matumaini ya kutajirika kwa haraka ingawa kazi yenyewe ina hatarisha maisha.

Wachimbaji migodi hao, wengi wao wanategemea watoto walioacha elimu wakijaribu kutafuta maisha kusaidia familia zao.

Africa Eye inafuatilia simulizi ya Justice Afekey, kuanzia alioacha shule hadi alipotajirika ghafla kwa kufanyakazi katika moja ya migodi haramu.