Walinzi wa mwambao wa Ugiriki walivyofyatua risasi kuwazuia wahamiaji kuendelea na safari
Picha za video zimepatikana za walinzi wa mwambao wa Ugiriki wakifyatua risasi ndani ya eneo la bahari karibu na mashua ya wahamiaji, na kuwazingira kujaribu kuwalazimisha warudi nyuma Uturuki walikotoka.
Maelfu ya wahamiaji wameelekea katika mataifa ya Muungano wa Ulayua baada ya serikali ya Uturuki kutangaza kuwa itafungua mipaka yake na Ugiriki.