Darfur yasubiri haki baada ya mauaji ya 'kwanza ya kimbari katika karne ya 21'
Serikali mpya ya Sudan, iliyoingia madarkani baada ya kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Omar al-Bashir, imesema wale wanaotafutwa na mahakama ya kimataifa ya ICC, watafika mahakamani kukabiliana na mashtaka ya mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur.
Uamuzi huo unafungua njia kwa rais wa zamani kupelekwa the Hague.