Rais Salva Kiir na Riek Machar waafikiana, je hili linamaanisha nini kwa usalama wa Sudan?
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir anasema yeye na kiongozi mkuu wa zamani wa waasi Riek Machar wameafikia makubaliano ya kuunda serikali ya umoja iliyocheleweshwa kwa muda mrefu.
Kiir na Riek Machar, ambaye sasa ni kiongozi wa upinzaji, walikutana siku tatu zilizopita katika mji mkuu Juba kutafuta suluhu la migogoro ambayo ilizuia kuunda serikali hiyo ya umoja wa kitaifa.
Huku tarehe ya mwisho ya kuundwa kwa serikali hiyo, Novemba 12 ikipita zamani, kulikuwa na wasiwasi wa kimataifa kwamba vita vinaweza kuanza tena.
Mwezi uliopita, viongozi hao wawili waliomba muda zaidi kuchelewesha kuundwa kwa serikali hiyo kwa siku 100 baada ya tarehe ya mwisho kupita.
Lakini hili linamaanisha nini sasa kuhusu amani na usalama ya Sudan Kusini?
Mwenzangu Caro Robi amemuuliza swali hilo mwanasheria Martin Oloo ambaye wakati mmoja alihudumu kama mshauri wa kisheria wa Rais Salva Kiir:
Na Caro Robi