Je unachukua hatua gani kukabiliana na vitendo vya ubakaji kwenye jamii yako?
Katika haba na haba wiki hii, tunaangazia swala la ubakaji nchini Tanzania, ambapo kwa mujibu wa takwimu za taifa (NBS ) zinaonesha Kuongezeka kwa kuripoti visa vya ubakaji amabapo mwaka 2005 viliripotiwa visa zaidi ya 5000, na hadi kufikia mwaka 2017 vimeripotiwa visa zaidi ya 7000. Sasa tunahoji je unachukua hatua gani kukabiliana na vitendo vya ubakaji katika eneo lako?