Ni kwanini jamii ya Herero hujivunia vazi lake maalumu Namibia?

Maelezo ya video, Vazi maalumu linalojivuniwa jamii ya Herero Namibia

Namibia ilikuwa ni koloni la Ujerumani kwa zaidi ya karne na katika miaka ya mwanzo ya 1900 jamii za watu wa Herero na Nama zilipambana na Wajerumani na kukukabiliwa na athari za maafa.

Watu wapatao 65,000 wa kabila la Herero waliuawa na vikosi vya Ujeruman.

Kila mwaka wtu wa Herero huwakumbuka wale waliouawa katika vita hivyo kwa sherehe maalumu. Na wanawake huvaa gauni maalumu ambalo ni maalumu kwa utamaduni wa Herero.

Kipindi cha Watoto cha BBC Afrika cha What’s New? kilikutana na Ngutjiua, msichana mdogo wa kabila la Herero nchini Namibia ambaye alielezea umuhimu wa gauni hilo.