Wahamiaji hupoteza mabilioni ya fedha kwa mawakala wakituma fedha nyumbani

Maelezo ya video, Wahamiaji wanapoteza mabilioni ya fedha kwa mawakala wakituma fedha nyumbani

Wafanyakazi wahamiaji, wengi wanaolipwa fedha kidogo, hutuma mabilioni ya dola nyumbani wanakotoka kwa ajili ya kusaidia familia zao. Lakini kiasi kikubwa cha fedha hizo huchukuliwa kama ada ya kutuma pesa. Mwaka 2018 gharama za kutuma fedha zilikuwa kubwa zaidi ya jumla ya misaada inayotolewa kwa bara la Afrika kutoka kwa serikali za kigeni.

Lakini je kwa nini gharama ziko juu na je zinaweza kupunguzwa?