Mwendesha baiskeli afariki akijaribu kumkwepa ndege aina ya Kwenzi Australia

A magpie flies over a road in bushland

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndege aina ya Kwenzi kwa kawaida huwa tishio kwa wanedesha basikeli nchini Australia

Mwanamume mmoja raia wa Australia amefariki katika ajali ya baiskeli wakati akijaribu kukwepa ndege aina ya Kwenzi aiyekuwa akipepea juu yake.

Mwendesha baiskeli huyo mwenye umri wa miaka 76 alipata jareha la kichwa Jumpaili wakai alipopoteza muelekeo kutoka barabarani na kujigonga na uzio kusini mwa Sydney, polisi wamesema.

Licha ya jitihada za wahudumu wa afya kumuokoa, jamaa huyo alifariki alipofikishwa hospitalini baadaye.

Ndege hao kwa kawadia ni tishio nchini Australia wakati wa msimu wa machiouko na mara nyingi husababisha majeruhi kwa wanedesha baiskeli na hata wapita njia, lakinini nadra kwa waathiriwa kufariki.

Polisi wamesema watawasilisha ripoti ya mpasuaji maiti baada ya tukio hilo huko Wollongong, New South Wales.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba kumeshuhudiwa mashambulio mengine kadhaa ya ndege hao Kwenzi katika bustani kulikotokea ajali hiyo.

Kwenzi wa Australia ni tofauti na ndege wa Ulaya ambao wana jina sawa. Wakati wa msimu wa kujamiiana, ndege hao huwa wakali na huwashambulia binaadamu wanaopita katika maeneo wanakoishi.

A sign in a park reads: Attention: Please be aware of aggressive magpies

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndege hao huwashambulia sana wakaazi wakati wa msimu wa machipuko

Mapema mwezi huu, serikali ya mtaa huko Sydney ilizusha mzozo wakati maafisa wa wanyama pori walipompiga risasi Kwenzi mkubwa, aliyewatishia wakaazi kwa miaka kadhaa.

Ndege huyo mkali aliwashambulia watu kadhaa na kusababisha baadhi kujeruhiwa na kupelelekwa hospitalini.

Mkaazi mmoja pia alipatwa na mshtuko wa moyo baada ya kukabiliana na ndege huyo, shirika la habari nchini Australia linaripoti.

Maafisa kwa wakati huo, walitetea uamuzi wa kumuua Kwenzi huyo mkubwa. Ndege huyo hulindwa kwa sheria nchini lakini anaweza kudhibitiwa kwa hiari ya maafisa wa utawala.

line

Huenda pia ukavutiwa na hii:

Maelezo ya video, Ndege ya abiria yatua kwa ghafla baada ya kugongana na kundi la ndege