Ndege ya abiria yatua kwa ghafla Urusi baada ya kugongana na kundi la ndege
Ndege ya abiria ya Urusi imelazimika kutua kwa dharura kwenye shamba la mahindi karibu na jiji la Moscow baada ya kugonga kundi la ndege.
Watu ishirini na watatu wamejeruhiwa katika tukio hilo, ambalo limesababisha ndege kutua huku injini yake ikiwa imezima na gia yake kutua ikirudi nyuma, wamesema maafisa wa afya.