Vikwazo vya Marekani vinaiathiri vipi Iran?

Maelezo ya video, Vikwazo vya Marekani vinaiathiri vipi Iran?

Ni mwaka mmoja tangu rais Donald Trump aanze kuidhinisha upya vikwazo dhidi ya Iran, miezi mitatu baada ya kutangaza kujitoa kutoka mkataba wa nyuklia. Utawala wa Trump umevitaja vikwazo hivi kuwa vikali mno kuwahi kuidhinishwa dhidi ya nchi hiyo. Inasema serikali tu ndio iliolengwa, na sio raia wa kawaida. Lakini vikwazo vinaathiri maisha ya kawaida nchini Iran na vitu hivi vitano vinaeleza athari yake.