DJ Wiwa: Atumia miguu kuzungusha santuri

Maelezo ya video, Winfred Wanjiku 'Ulemavu wangu sio kizingiti cha kutokuwa DJ wa kimataifa'

Winfred Wanjiku, mwenye umri wa miaka 23, alizaliwa na utandio wa ubongo nchini Kenya. Wanjiku maarufu kama 'Dj Wiwa Queen of Decks' hutumia miguu kuyakimu maisha yake. Wanjiku ana uwezo wa kucheza santuri kwa miguu na hata kuandika kupitia mdomo wake. Paula Odek alimtembelea na kutuandalia taarifa hii