Raphael Ongangi: Mkewe Mkenya aliyetekwa nyara Tanzania na kupatikana Mombasa azungumza

Maelezo ya video, Mkewe mfanyabiashara wa Kenya aliyetekwa nyara Tanzania na kuachiliwa Mombasa azungumza

Anasema kwamba alihisi kama alivyohisi siku ya ndoa yake alipokutana na mumewe.

Kwa mujibu, wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini Kenya na Tanzania, watu wasiojulikana waliwafuatilia wanandoa hao na kisha kulizuia gari yao na kumchukua bwana huyo na kuondoka naye.