BBC Africa Eye: Wizi wa madawa wafichuliwa Uganda
Hebu fikiria, kuishi katika nchi ambako madaktari na maafisa wa madawa wanaiba dawa zinazookoa maisha, na zilizolengwa kupewa wagonjwa - ulafi wa wahudumu wa afya unaozidi wajibu wao wa kuwajali wagonjwa.
BBC Africa Eye imefanya upekuzi nchini Uganda kufichua jinsi wafanyakazi wa afya nchini humo walivyojitosa katika mitandao ya uhalifu.
