Kwa Picha: Mashabiki walivyoishangilia Simba

Soka ya kasi, pasi fupi na uharaka wa wachezaji wa Simba kila walipopata mpira ilitosha kuitikisa Sevilla katika mchezo huo tofauti na watu walivyotarajia.

Uwanja wa taifa wa ulifurika mashabiki waliyojitokeza kujione meche kati ya Simba na Sevilla.
Maelezo ya picha, Uwanja wa Taifa Dar es salaam ulifurika mashabiki waliyojitokeza kuonea mechi kati ya Simba SC na Sevilla FC.
Baadhi ya mashabiki walikuwa na mabango yaliyoandikwa kwa lugha ya Kihispania.
Maelezo ya picha, Baadhi ya mashabiki walikuwa na mabango yaliyoandikwa kwa lugha ya Kihispania.
Mashabiki walijitokeza wakiwa wamevalia kila aina ya mapambo kuashiria usuhuba wao kwa timu ya nchumbani.
Maelezo ya picha, Mashabiki walijitokeza wakiwa wamevalia kila aina ya mapambo kuashiria usuhuba wao kwa timu ya nchumbani.
Wengine walilazimika kutoa mashati joto lilikuwa limepanda uwanjani wakati wa mechi hiyo ya kusisimua.
Maelezo ya picha, Matukio kadhaa yaliyojitokeza ndani na nje ya uwanja yaliashiria kiwango cha ubora wa Simba. Baadhi ya mashabiki walilazimika kutoa mashati wakati joto lilipopanda uwanjani wakati wa mechi hiyo ya kusisimua.
Baba na watoto wao pia hawakuachwa nyuma
Maelezo ya picha, Wakubwa kwa wadogo walijitokeza kujionea mechi kati ya Simba na Sevilla.
Wachezaji wa Simba kabla ya mechi dhidi yao na Sevilla kuanza.
Maelezo ya picha, Muda mfupi kabla ya mechi kuanza mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania msimu huu walipiga picha.
Mchezaji wa Simba Meddie Kagere akifanya akionesha umahiri wake uwanjani.
Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Simba,Meddie Kagere akionesha umahiri wake uwanjani.
Mavazi yao yalikuwa tofauti kabisa na wengine lakini yanaonesha wazi uzalendo wao kwa Timu ya Simba
Maelezo ya picha, Mavazi yao yalikuwa tofauti kabisa na wengine lakini yanaonesha wazi uzalendo wao kwa Timu ya Simba
Wengine walikuwa wametekwa na shughuli iliyokua uwanjani lakini shabiki huyo alipata wasaa wa kuonesha wapiga picha wetu upendo wake kwa timu yake.
Maelezo ya picha, Wengine walikuwa wametekwa na shughuli iliyokua uwanjani lakini shabiki huyo alipata wasaa wa kuonesha wapiga picha wetu upendo wake kwa timu yake.
Wachezaji wa Sevilla
Maelezo ya picha, Wachezaji wa Sevilla wakipokea Kombe la ushindibaada ya kuifunga Simba mabao 5-4