Faustine Ndugulil: Unene wa kupindukia waleta hofu Tanzania

kitambi

Chanzo cha picha, Getty Images

Mamlaka ya afya nchini Tanzania, imepata hofu ya ongezeko la watu wenye uzito mkubwa.

Naibu waziri wa afya , maendeleo ya jamii , jinsia, wazee na watoto, Faustine Ndugulile amesema kuwa sasa ni zaidi ya asilimia kumi ya watanzania wanasumbuliwa na tatizo hilo la uzito wa kupindukia.

Waziri huyo ameainisha kuwa ongezeko la kuenea kwa magonjwa yasiyoambukiza imeleta changamoto na kutoa tahadhari kuwa idadi hiyo kubwa inaweza kusababisha madhara makubwa kwa wananchi wa taifa hilo.

Aidha ameainisha kuwa tatizo la uzito uliopindukia ni kubwa kwa wanaume na wanawake wa maeneo ya mjini kuliko vijijini.

Huku changamoto ya vyakula vyenye virutubisho kuongeza kesi ya tatizo hilo kwa kiwango kubwa .

unene

Chanzo cha picha, Getty Images

Naibu waziri Faustine Ndugulile alieleza hayo wakati anajibu swali la nyongeza lililoulizwa bungeni na Zainabu Mwamwindi aliyeuliza kama kuna uhitaji wa kuwawezesha maafisa wa lishe kwa sababu ya ongezeko la utapia mlo.

lishe

Chanzo cha picha, Getty Images

Utapia mlo ni tatizo kubwa miongoni mwa watoto nchini Tanzania, na jitihada gani ambazo serikali inazifanya ili kuboresha hali hiyo ikiwa ni pamoja na kuwawezesha afisa wa afya ya chakula .

Naibu waziri amesema miongoni mwa jitihada ambazo zimechukuliwa na serikali ni pamoja na kuwa na mpango wa kazi wa lishe kwa kuangalia vipaumbele katika maeneo sita.

Mambo hayo ni pamoja na watoto wachanga, wajawazito, lishe ya watu wazima na kuangalia usimamizi wa upatikanaji wa chakula.