Mwalimu bora duniani apania kuwawezesha wasichana kupenda masomo ya sayansi

Maelezo ya video, Mwalimu wa Sayansi nchini Kenya ashinda tuzo ya dunia ya mwalimu bora zaidi.

Mwalimu wa sayansi Peter Tabichi kutoka eneo la kijijini nchini Kenya , ambaye hutoa sehemu kubwa ya mshahara wake kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi maskini zaidi , ameshinda tuzo la dola milioni moja ($1m ) kwa kuwa mwalimu bora zaidi duniani.