Anne-Marie alipoteza watoto wake wanne na mumewe wakati wa mauaji ya kimbari
Anne-Marie alipoteza watoto wake wanne na mumewe wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.Mwanaume mmoja kwa jina Celestin alivamia nyumbani kwa Anne-Marie na washambuliaji na kuwaua watoto wake wawili.
Washambuliaji walikua na marungu na mapanga.Celestin alichomoa panga na kukata shingo za watoto wawili.
Pamoja na aliyoyapitia Anne-Marie,Kasisi wa kikatoliki alimshawishi Anne-Marie kumsamehe Celestin.
Celestin amejutia dhambi aliyoifanya.