Fahamu miji kumi bora zaidi kuishi duniani ?

Maelezo ya video, Ni mji gani mzuri zaidi duniani kuishi?

Una mpango wa kuhama? Kama jibu lako ni ndio, basi video hii itakufaa.

Hii ni miji mizuri zaidi kuishi duniani kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na kampuni ya Mercer kwa kuzingatia vigezo kadhaa vya hali ya maisha.

Kampuni hiyo imelinganisha jumla ya miji 231 duniani kwa kuangazia masuala kama vile, viwango vya uhalifu, elimu, afya, makaazi na uhuru wa kibinafsi.