Nyangumi aliyefariki ufilipino alikuwa amemeza kilo 40 za plastiki akidhani ni chakula
Mataifa mengi ya bara Asia yamelaumiwa kuchangia pakubwa katika uchafuzi wa mazingira kutokana na matumizi holela ya plastiki -yakiwemo UChina, Indonesia, Philippines, Vietnam na Thailand -kwa asilimia zaiid ya 60 ya uchafu wa plastiki unaoharibu mazingira ya baharini kwa mujibu wa ripoti ya 2015 ya wanamazingira waitwao Ocean Conservancy na wakishirikiana wao. Mataifa kadhaa ya Afrika yameweka marufuku ya matumizi ya baadhi ya bidhaa za plastiki lakini bado kuna ulegevu katika kutekelezwa kwa sheria hizo. Je, kipi kifanyike kudhibiti taka za plastiki? Tueleze kwenye ukurasa wa facebook, bbcswhili.