Shambulio katika misikiti New Zealand: Ambulensi zawasili Hospitali

Maelezo ya video, Maafisa wa huduma ya dharura wawashughulikia walioshambuliwa mjini Christchurch New Zealand.

Risasi zimesikika karibu na mskiti wa Al Noor katika mji wa Christchurch, New Zealand, vyombo vya habari vinaripoti wakatipolisi wakionya kuhusu "tukio kuu".

Walioshuhudia wanasema wameona watu kadhaa wameuawa. Polisi imewaonya watu kuepuka kufika katika eneo hilo.