Toi Market: Moto wateketeza mali ya thamani isiyojulikana Nairobi

Wafanyabiashara wanahesabu hasara baada ya mali ya thamani isiyojulikana kuteketea Jummane alfajiri katika soko la Toi mjini Nairobi

moto toi

Chanzo cha picha, Oliver Koech

Maelezo ya picha, Moto umewaka mwendo wa saa tisa Jumanne alfajiri katika soko la Toi mjini Nairobi.
moto toi

Chanzo cha picha, Oliver Koech

Maelezo ya picha, Ni soko maarufu linalofahamika kwa uuzaji wa bidhaa kukuu zikiwemo nguo za mtumba, lakini pia bidhaa nyingine kama mbao na vifaa vya elektroniki.
moto toi

Chanzo cha picha, Oliver Koech

Maelezo ya picha, Muuzaji mmoja Charlie Chaplin ameiarifu BBC kwamba aliamshwa alfajiri kwa simu akiarifiwa kwamba moto umezuka na alilazimika kukimbia kwenda katika soko hilo. Kwa sasa anasema anakadiria hasara ya mamilioni ya shilingi za Kenya.
moto toi

Chanzo cha picha, Oliver Koech

Maelezo ya picha, Mwandishi habari aliyefika katika eneo hilo Oliver Koech, anasema baadhi wamelalamika kuhusu kujivuta kwa idara za zima zoto kukabiliana na moto huo kwa wakati mzuri na kuudhibiti kabla ya kusambaa kama ulivyosambaa na kuiharibu sehemu kubwa ya soko hilo. Sio mara ya kwanza magari ya zima moto kushutumiwa nchini kwa kushindwa kudhibiti mikasa ya moto kwa muda muafaka na licha ya kuwa na vifaa vipya.
moto toi

Chanzo cha picha, Oliver Koech

Maelezo ya picha, Makazi yasiyo rasmi kama vijiji yanakuwa hayana mpangilio mzuri, nyumba husongamana sana na hakuna njia za katikati, hivyo magari ya zima moto hushindwa kuingia ndani zaidi. Kufikia saa moja asubuhi ya leo, baadhi ya wauzaji walikuwa wakijaribu kukusanya masalio ya mali zao katika eneo hilo la Toi.
Moto Toi

Chanzo cha picha, Oliver Koech

Maelezo ya picha, Wauzaji wengi wanahesabu hasara ya thamani ya mali isiyojulikana katika soko hilo lililo karibu na mtaa mkubwa wa mabanda Kibera mjini Nairobi.
Moto Toi

Chanzo cha picha, Oliver Koech

Maelezo ya picha, Wanasema ni pigo kubwa, na hawajui la kufanya kutokana na kwamba walitegemea biashara katika soko hilo kujikumu maisha.