Wafanyikazi wanapinga pendekezo la uongozi wa uwanja huo kupewa kampuni ya ndege ya Kenya Airways.

Maelfu ya wasafiri wa ndege waliokuwa wakisafiri maeneo tofauti duniani walijipata bila pa kwenda siku ya Jumatano baada ya wafanyikazi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA nchini Kenya kugoma.

Uwanja wa ndege wa JKIA
Maelezo ya picha, Ilikua hakuna kutua au kupaa kwa ndege katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta
Wengi wa wasafiri walikua hawajapata suluhu kwasababu safari nyingi zilikuwa zimefutiliwa ama kucheleweshwa.
Maelezo ya picha, Wengi wa wasafiri walikua hawajapata suluhu kwasababu safari nyingi zilikuwa zimefutiliwa ama kucheleweshwa.
Katibu mkuu wa muungano wa wahudumu uwanja wa ndege Moss Ndiema alikatwa na baadaye na kufikishwa mahakamani kwa kuongoza mgomo usio halali kwani mahakama ilikuwa imetoa uamuzi usitishwe.
Maelezo ya picha, Katibu mkuu wa muungano wa wahudumu uwanja wa ndege Moss Ndiema alikatwa na baadaye na kufikishwa mahakamani kwa kuongoza mgomo usio halali kwani mahakama ilikuwa imetoa uamuzi usitishwe.
Waliyoathirika zaidi na mgomo huo ni abiria ambao walikwama kwa saa kadhaa.
Maelezo ya picha, Waliyoathirika zaidi na mgomo huo ni abiria ambao walikwama kwa saa kadhaa.
Abiria wengine walikabiliwa na matatizo ya kiafya.
Maelezo ya picha, Abiria wengine walikabiliwa na matatizo ya kiafya.
Baadhi ya wahudumu wa ndege pia walijipata katika mgomo huo.
Maelezo ya picha, Baadhi ya wahudumu wa ndege pia walijipata katika mgomo huo.
Hakuna ndege yoyote iliyotua katika uwanja huo mkubwa katika kanda ya Afrika mashariki ambao unaohushughulikia ndege za abiria 120 kila siku.
Maelezo ya picha, Hakuna ndege yoyote iliyotua katika uwanja huo mkubwa katika kanda ya Afrika mashariki ambao unaohushughulikia ndege za abiria 120 kila siku.
Shirika la ndege la Kenya Airways limetoa wito kwa wasafiri kuepuka uwanja huo au kubadilisha ndege zao bila gharama yoyote.
Maelezo ya picha, Shirika la ndege la Kenya Airways limetoa wito kwa wasafiri kuepuka uwanja huo au kubadilisha ndege zao bila gharama yoyote.
Ilikuwa afueni kwa baadhi yao baada ya wanajeshi wa anga wa KDF kuletwa ili kusaidia katika ukaguzi.
Maelezo ya picha, Ilikuwa afueni kwa baadhi yao baada ya wanajeshi wa anga wa KDF kuletwa ili kusaidia katika ukaguzi.