Mwewe aliyekwama ndani ya theluji aokolewa
Mwewe huyu hajatua hapa kama unavyoona bali ameshindwa kuruka baada ya theluji kuganda katika mabawa yake.Kwa bahati nzuri aliokolewa na maafisa wa hifadhi ya wanyama ya Michigan,nchini Marekani. Maafisa hao wanaamini ndege huyo alijipata katika hali hiyo alipokua akijaribu kushika samaki. Hatahivyo amefanikiwa kuruka tena baada ya theluji iliyoganda kwenye mabawa yake kuyeyushwa.
