Mkunga anayewakanda waja wazito kwa kuwakanyaga

Maelezo ya video, Wataalaamu wanaonya kuhusu hatari ya kuwakanda waja wazito

Ni utamaduni unaondamana na wakati wa mama kujifungua mtoto katika jamii nyingi Barani Afrika. Huku gharama ya huduma ya matibabu ya afya ya uzazi ikiendelea kuwa ghali, wanawake wengi wamekimbilia kwenye huduma za wakandaji na wakunga wa kiasili ambao huwapa huduma zao hususan wakati wa uja uzito, kujifungua na baada ya kujifungua. Wataalaamu wa afya sasa wanaonya kwamba Huduma hii ya kuwakanda wanawake waja wazito huenda ikahatarisha afya yao na watoto.

Kwa mengi zaidi katika makala ya BBC Maisha, tafuta BBCSwahili kwenye Youtube.