Tundu Lissu: 'Chama kikisema mimi nafaa, niko tayari kuwa rais Tanzania'
Mmoja wa wanasiasa wa upinzani wa Tanzania ambaye tayari ametangaza kutaka kuwania urais wa nchi hiyo mwakani amesema nafasi hiyo itategemea makubaliano ndani ya chama chake. Tundu Lissu kutoka chama kikuu cha upinzani CHADEMA ambaye kwa sasa anatibiwa nchini Ubelgiji baada ya kujeruhiwa kwa risasi mwaka 2017 amesema vikao vya chama ndio vitatoa mwelekeo wa nani atasimama mwaka 2020. Amekuwa akizungumza na Zuhura Yunus mjini London ambapo alipata mualiko wa kuzungumza na kipindi cha BBC cha HardTalk.
