Fikisha App: Programu tumishi inayokuletea kondomu ulipo Kenya

Maelezo ya video, App inayokuletea kondomu ulipo Kenya

Je fikra za kununua mipira ya kondomu dukani zinakutia hofu ama aibu? Je unajipata ukinunua karibu kila kitu katika duka la jumla ama lile la dawa ilki ujipatie mipira ya kondomu?

Sasa kuna suluhu.

Kampuni moja nchini Kenya kwa jina Ad Visions imeanzisha programu tumishi kwa jina 'Fikisha' inayoweza kutumika kununua mipira tofauti ya kondomu na kukuwasilishia pale ulipo.

Video: Abdalla Dzungu, BBC

Unaweza kusoma pia: