Nadya Ali Kassim: Uchoraji wa henna si wa wazee pekee

Maelezo ya video, Uchoraji wa henna unavyowavutia na kuwafaa vijana Mombasa, Kenya

Sanaa ya uchoraji wa henna imekuwepo kwa miaka mingi miongoni mwa wanawake wa pwani ya Afrika Mashariki.

Na sasa baadhi ya vijana wameanza kujitosa katika biashara hiyo.

Mmoja wao ni Nadya Ali Kassim kutoka mji wa Mombasa Kenya, na alieleza BBC Mitikasi unachohitaji ili kunawiri katika biashara hiyo