Uchaguzi Marekani 2018: Mambo muhimu kuhusu uchaguzi wa katikati ya muhula

Maelezo ya video, Uchaguzi Marekani 2018: Mambo muhimu kuhusu uchaguzi wa katikati ya muhula

Miaka miwili baada ya Donald Trump kushinda urais na kuingia White House, Wamarekani wanashiriki tena uchaguzi wa katikati ya muhula, wakati huu wakiwachagua wawakilishi wao Bunge la Congress.

Jinsi watakavyopiga kura itakuwa na athari kubwa katika kipindi kilichosalia cha uongozi wa Trump.

Hapa, tumekuandalia mambo muhimu unayofaa kuyafahamu kuhusu uchaguzi huo.