'Kimondo cha nyota' Tanzania
Kupiga picha kwenye kimondo cha Mbozi ni tukio la kipekee kwenye kivutio cha utalii kilichopo wilayani Mbozi, mkoa wa Songwe, Nyanda za Juu Kusini nchini Tanzania. Kimondo cha Mbozi kinakadiriwa kuwa na uzito wa tani 12 na ni cha nane kwa ukubwa duniani.
Ni cha pili Afrika baada ya kimondo cha Hoba chenye tani 60. Kimondo cha Hoba kilichopo nchini Namibia ndicho kikubwa zaidi Afrika na duniani.
Mpiga picha: Eagan Salla