Mo Dewji: Watu walionikamata walikuwa na lafudhi ya taifa la kigeni

Maelezo ya video, Mo Dewji aliporudi nyumbani

Mo Dewji, bilionea Mtanzania aliyetekwa na watu wasiojulikana Alhamisi wiki iliyopita, amerejea nyumbani salama.

Katika ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wa Twitter wa kampuni yake, amesema: "Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama."

Picha: Lazaro Mambosasa