MV Nyerere: Ni vipi tunaweza kuzuia ajali za feri?

Maelezo ya sauti, MV Nyerere: Ni vipi tunaweza kuzuia ajali za feri?

Mamia ya watu ambao wamewapoteza wapendwa wao kwenye mkasa wa Mv Nyerere wanatarajiwa kupewa dola 400 kama fidia. Idadi ya waliofariki kutokana na mkasa wa MV Nyerere kwa sasa inaripotiwa kuwa watu 220. Jitihada kwa sasa zinaendelea za kuipindua na kuivuta feri hiyo. Kuna maswali mengi kuhusu wajibu wa nahodha wa feri na maafisa wengine wakati kisa kama hiki kinatokea. Pia mkasa kama huo unaweza kuepukwa kwa njia gani. Nahodha Ibrahim Mbiu Bendera ni mtaalamu wa sheria za usafiri wa baharini.