Kwa nini ulanguzi wa dawa bado ni tatizo Tanzania?

Maelezo ya sauti, Mkutano kuhusu kupambana na dawa za kulevya wafanyika Dar es Salaam

Mkutano wa 28 wa Umoja wa mataifa Kanda ya Afrika kwa wakuu wa vyombo vinavyopambana na biashara ya dawa za kulevya unafanyika jijini Dar es Salaam Tanzania.

Mkutano huu unaohudhuriwa na washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi 55 umelenga kuweka mipango ambayo nchi za Afrika zinaweza kutekeleza kupambana na matumizi ya dawa za kulevya.

Wakati baadhi ya raia wa Afrika kusini wakisheherekea kuhalalishwa kwa matumizi ya Bangi, Serikali ya Tanzania imesema imedhibiti matumizi ya dawa za kulevya kwa asilimia 90.Hata hivyo changamoto ipo, kwani bado kuna matumizi ya aina ya dawa za hospitalini ambazo huwa kilevi kwa wale wanaozitumia vibaya.

Kelvin Richard Muzo, ni mwenyekiti wa mfuko uitwao Me and You ambao unalenga kutoa elimu, kupambana na uraibu wa madawa na pombe.