Je damu ya vijana ndio tiba ya kuzeeka?
Utafiti mpya unaonyesha kuwa damu ya vijana inaweza kuruhusu binaadamu kuishi maisha yasiokumbwa na magonjwa yanayotokana na uzee kama saratani na matatizo ya kusahau au ugonjwa wa moyo. Wataalamu kutoka University College London, waliochapisha utafiti wao katika jarida la ‘Nature’, wanasema majaribio zaidi yanahitaji kufanywa kwa wanyama kuamua iwapo majaribio yafanyiwe binaadamu katika siku zijazo.
