Melida Auma: Nataka ukweli ujulikane kuhusu mauaji ya Sharon Otieno
Taarifa za kisa cha mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu Sharon Otieno zimetawala vichwa vya habari nchini Kenya, kila siku kukitokea jipya kuhusu mauaji hayo.
Bi Otieno alikuwa ametekwa pamoja na mwanahabari wa shirika la Nation Media Group Barrack Oduor kabla ya mwili wake kupatikana ukiwa umetupwa vichakani Oyugis katika jimbo la Homa Bay.
Mamake Sharon, Melida Auma, amesema anataka kujua ukweli kuhusu mauaji ya mwanawe.
Video: Victor Kenani na Ken Mungai, BBC