Mzee Andrew Mbanga: Fundi wa Kinondoni, Dar es Salaam aunda bajaj ya kipekee Tanzania

Maelezo ya video, Mzee Mbaga: Fundi wa Kinondoni, Dar es Salaam aunda bajaj ya kipekee

Mzee Andrew Mbanga , ambaye ni mhandisi wa kujitegemea eneo la Kinondoni, Dar es Salaam, ameunda bajaj inayoweza kuwabeba abiria sita.

Ameiunda bajaj hiyo kwa kutumia vyuma na vipuri ambavyo havitumiki. Lengo lake ni kuzalisha bajaj za aina hiyo kwa wingi ingawa bado hajapata kibali.

BaJajI hii aliyoipa Jina la Mbanga Ina uwezo wa kubeba kilo elfu moja ikiwa ni ubunifu ulio mchukua miezi sita kukamilika akiunda vyuma vya aina mbali mbali hadi kukamilisha wazo lake.

Tayari BaJajI hii umepata mteja na anataka kutengenezewa nne zaidi ila Mbunifu huyu hawezi kutengeneza zaidi kabla hii ya kwanza haijapata kibali.

Video: Eagan Salla na Shedrack Mwansasu, BBC

Unaweza kusoma pia: