BBC Africa Eye: Kituo cha kurekebisha tabia ambapo wagonjwa huteswa Kenya

Maelezo ya video, Uchunguzi wa BBC Africa Eye umefichua kituo cha kurekebisha tabia ambapo wagonjwa huteswa

Uchunguzi wa BBC Africa Eye umefichua kuwa wanawake na wanaume wa kisomali wamekuwa wakifanyiwa mateso na kunyanyaswa katika vituo vya kurekebisha tabia Afrika Mashariki. Vituo hivyo vinadaiwa kuwa vinawarekebisha wale wanaokwenda kinyume na utamaduni wa kisomali na dini, vikiwashutumu kutumia mihadarati na kuwa na tabia zisizo za kiislam. Lakini kama alivyobaini Jamal Osman wanafanyiwa mateso makali.