Kitanzini: Eneo lililopata jina kutokana na kitanzi cha Mjerumani

Maelezo ya video, Kitanzini: Eneo lililopata jina kutokana na kitanzi cha Mjerumani

Maeneo mengi Afrika Mashariki unapotaja majina ya mahala fulani, mara nyingi huendana na sifa za eneo hilo.

Huko mkoani Iringa nyanda za juu Kusini mwa Tanzania, kuna eneo lijulikanalo kama kitanzini, likiwa maarufu kwa wizi na ukabaji.

Eneo hilo lilikua ni sehemu ya kujinyongea watu kipindi cha ukoloni, hivyo wengi huamini damu ya watu walionyongwa ni matokeo ya matendo yanayoendelea hivi sasa.

Mwandishi wetu Eagan Salla alitembelea eneo hilo na kuzungumza na watu ambao wana kumbukumbu za kitanzi hicho.