Buzz Aldrin: Mtu wa pili kutembea kwenye Mwezi awashtaki wanawe

Alikuwa ni mmoja wa watetezi wakuu wa binadamu kupeleleza katika sayari ya Mars

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bw Aldrin ni mmoja wa watetezi wakuu wa binadamu kupeleleza katika sayari ya Mars
Muda wa kusoma: Dakika 3

Mwanaanga maarufu kutoka Marekani Buzz Aldrin amewashtaki watoto wake wawili na meneja wa zamani wa biashara zake akidai kwamba waliiba pesa zake.

Aidha, anadai walimharibia sifa ambazo amejizolea katika maisha yake.

Kesi hiyo, ambayo ilifichuliwa Jumatatu, iliwasilishwa katika mahakama moja mjini Florida wiki moja baada ya watoto wake kuwasilisha ombi mahakamani wakitaka waruhusiwe kuchukua udhibiti wa fedha zake.

Jamaa zake walikuwa wamemwambia jaji kwamba anahitaji mlezi wa kumwakilisha kisheria kwa sababu uwezo wake wa "kufikiria umeshuka sana".

Mzee huyo wa miaka 88 alikuwa mtu wa pili kuwahi kutembea kwenye Mwezi.

Katika mahojiano na gazeti la Wall Street Journal wiki iliyopita, Aldrin ambaye ni kanali mstaafu wa jeshi la wanahewa la Marekani alisema: "Hakuna mtu atakayekaribia kufikiria kwamba ninaweza kuwekwa chini ya mlezi."

Kwenye kesi hiyo, anadai kwmaba mwanawe wa kiume, na binti yake pamoja na meneja wake wa zamani Christina Korp pia walivuruga uhusiano wake wa kimapenzi na watu wengine na kumzuia kuoa tena.

Mzozo unahusu zaidi usimamizi wa kampuni yake ya kibinafsi, Buzz Aldrin Enterprises, na shirika la hisani kwa jina ShareSpace Foundation.

Katika ombi waliloliwasilisha mahakamani, wanawe Andrew Aldrin, 60, na Janice Aldrin, 60, walisema baba yao hivi karibuni ameanza kujihusisha na marafiki wapya ambao wanajaribu kumpotosha na kumtenganisha na familia yake.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Walisema pia kwamba amekuwa akitumia pesa kwa "kasi ya kushangaza."

Bw Aldrin kwenye kesi yake anadai kwamba mwanawe wa kiume na Bi Korp wamechukua udhibiti wa fedha zake bila idhini - ikiwa ni pamoja na turathi za kutoka anga za juu pamoja na vitu vingine vyake vya thamani kubwa kuhusiana na anga za juu, vyote vya mamilioni ya dola.

Ameongeza kwamba walifanya hivyo kwa lengo la "kujifaidi wenyewe."

Kesi hiyo pia inadai wamekuwa wakimharibia jina kwa muda mrefu kwa kudai kwamba anakabiliwa na magonjwa magonjwa ya kiakili ya kupoteza kumbukumbu na kutojielewa, na pia anaugua ugonjwa wa Alzheimer.

Anamtuhumu mwanawe wa kiume kwa kumtumia vibaya mtu mzee kujifaidi kwa kumpokonya mali yake kwa kutumia njia za ulaghai.

Bintiye anamtuhumu kwa ulaghai na kwa kutotetea maslahi yake ya kifedha.

Mr Aldrin was honoured at a Veterans' Day parade last year

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Aldrin alituzwa wakati wa maonesho ya Mashujaa wa Jeshi Waliostaafu mwaka jana

Mwanawe wa kiumbe wa kwanza hajahusishwa katika kesi hiyo.

Mtaalamu wa afya ya kiakili aliyeteuliwa na mahakama anatarajiwa kumpima Bw Aldrin baadaye wiki hii.

Kupitia taarifa, watoto wake wamesema wamesikitishwa sana na kesi hiyo isiyo ya haki.

"Familia yetu bado ina umoja na azma yetu ya kufanya kazi kwa pamoja na kutatua matatizo pamoja na kutimiza mambo makuu bado ni kuu," watoto hao wa Aldrin wamesema.

President Richard Nixon met with the Apollo 11 crew during their quarantine after returning to earth

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Richard Nixon alikutana na wanaanga wa Apollo 11 walipokuwa bado wanaishi kwenye karantini baada yao kurejea duniani kutoka kwenye Mwezi

"Tunampenda na kumheshimu sana baba yetu na tunasalia na matumaini kwamba tunaweza kuyapita haya na kufufua uhusiano wetu mwema ambao ulijenga msingi wa haya yote."

Bw Aldrin alikuwa kwenye kundi la wanaanga wa Apollo 11 ambao mwaka 1969 walikuwa wa kwanza kabisa kufanikiwa kuwa na binadamu waliotembea kwenye Mwezi, ambapo wana anga wawili walifanya hivyo.

Mwenzake Aldrin alikuwa Neil Armstrong.

Astronaut Buzz Aldrin walks on the surface of the Moon near the leg of the Lunar Module (LM) "Eagle" during the Apollo 11 mission, 20 July 1969

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Buzz Aldrin akitembea kwenye Mwezi 20 Julai, 1969

Miaka ya karibuni, amekuwa akitetea sana kupelelezwa kwa sayari ya Mars na hatimaye kufanywa kwa juhudi za kuwapeleka binadamu wakaishi huko.

Wiki iliyopita, alitokea katika Baraza la Taifa la Anga za Juu katika ikulu ya White House ambapo Rais Donald Trump alitangaza kuundwa kwa Kikosi cha Anga za Juu ambacho kitahudumu kama tawi la sita la jeshi la Marekani.

Presentational grey line

Unaweza pia kusoma: