Kifaa kinachowasaidia wenye maradhi ya moyo Kenya
Ikiwa roho yako haipigi kwa kasi inayofaa, basi huenda unahitaji kifaa cha kudhibiti mapigo ya moyo, inayojulikana kama pacemaker.
Lakini upasuaji aina hiyo una gharama ya dola elfu tano, kiasi ambacho watu wengi barani Afrika hawawezi kumudu.
Takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka watu wapatao milioni mbili hufa kwa kutoweza kulipia upasuaji huu.