Kusambaza upendo kwa wagonjwa wa saratani katika siku ya wapendanao

Katika siku ya Valentine au siku ya wapendanao, mpabaji mashuhuri mjini Nairobi amejitolea kuwapamba bure wanawake waliopona saratani.

Wanawake warembeshwa nairobi
Maelezo ya picha, Wanawake waliwasili wakiwa wamevaa vitambara kichwani lakini waliondoka wakiwa wamerembeshwa vilivyo na kupewa wigi za bure.
Wanawake warembeshwa nairobi
Maelezo ya picha, Makumi kadhaa ya wanawake waliopona saratani, walipata fursa ya kujumuika na wenzao na kurembwa vilivyo katika kusambaza upendo siku ya wapendanao 'Valentine'
Diana Kwamboka
Maelezo ya picha, Diana Kwamboka mwenye umri wa miaka 35 amepona saratani ya matiti
Wanawake warembeshwa nairobi
Maelezo ya picha, Diana anasema anahisi vizuri kuhusu muonekano wake mpya, na zaidi kupata nywele mpya baada ya kupoteza nywele zake katika matibabu aliyokuwa anapokea.
Wanawake warembeshwa Nairobi
Maelezo ya picha, Je umeisherehekea vipi siku hii ya wapendanao?