Kwa Picha: Mwezi mkubwa wa kipekee washuhudiwa angani

Huu ni mkusanyiko wa picha za Mwezi mkubwa wa kipekee ulivyoonekana katika maeneo mbalimbali duniani.

The bright orange moon set against a deep blue cityscape of Madrid, Spain

Chanzo cha picha, Mehdi Amar

Maelezo ya picha, Tukio ambalo si la kawaida, Mwezi mkubwa wa kuangaza, ambao huitwa kwa Kiingereza "Super blue blood moon" (Mwezi Mkubwa wa Buluu na Damu) ulishuhudiwa Jumatano maeneo mengi duniani. Mehdi Amar alipiga picha hii Madrid.
The moon appears bright white between a United States of America flag and the Indiana capitol building

Chanzo cha picha, Usha Venkat

Maelezo ya picha, Hutokea wakati kupatwa kwa mwezi, kuwepo kwa mwezi wa buluu na kuwepo kwa mwezi mkubwa wa kuandama, vinapotokea vyote vitatu kwa pamoja. Usha Venkat alipiga picha hii Indiana, Marekani.
The supermoon is bright red as it appears over a cityscape featuring modern buildings in Singapore.

Chanzo cha picha, Abdul Rahman Yassin

Maelezo ya picha, Tukio hilo lilishuhudiwa na watu maeneo mbalimbali duniani, akiwemo Abdur Rahman Yassin, aliyepiga picha hii Singapore.
A "super blood blue moon" is seen behind an elephant statue during an eclipse at a temple in Bangkok, Thailand, 31 January, 2018.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Hapa, Mwezi unaonekana nyuma ya hekali moja Bangkok.
The super blue blood moon rises above the sky in Naypyitaw, Myanmar, 31 January 2018

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mwezi wa buluu hutokea kunapokuwa na mwezi wa mwandamo mara mbili kwa mwezi, nao mwezi mkubwa hutokea Mwezi unapokuwa karibu zaidi na Dunia. Hapa ni Myanmar.
The statue of liberty is seen with pink glowing moon, large around its base

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mwezi huo ulionekana mataifa ya magharibi kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miaka 150. Hapa ni New York.
Moon is pictured setting behind San Francisco skyline

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Maelezo ya picha, Mwezi hapa unaonekana mjini San Francisco, California.
The moon is seen during a lunar eclipse referred to as the super blue blood moon, in Jakarta on 31 January 2018.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Picha hii ya karibu ilipigwa Jakarta, Indonesia.
The super blue blood moon shines its blood red colours during a full eclipse above the Big A Sign of Angel Stadium in Anaheim, California

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Neno "damu" hutumiwa kueleza rangi nyekundu iliyokolea inayotokea miali ya jua inapopita katika anga ya Dunia na kuangaza kwenye Mwezi. Rangi hiyo hutokana na tukio ambalo pia hufanya anga kubadilisha rangi wakati wa kutua kwa jua, au anga mchana kusipokuwa na mawingu au vumbi kuonekana ya rangi ya samawati. Hapa ni Anaheim, California.
A super blue blood moon behind a mountain is seen from Longyearbyen, Svalbard, Norway, against a violet sky

Chanzo cha picha, AFP/getty

Maelezo ya picha, Baadhi ya miali hupitia anga ya Dunia na kufika Mwezini, na pia hujipinda kiasi na kuelekea kwenye Mwezi kidogo. Hili huondoa kiasi miali ya buluu na kuacha miali ya rangi nyekundu ikionekana zaidi. Hapa ni Svalbard, Norway.
Supermoon rises behind London's St Paul's cathedral

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwezi huo ulionekana pia Uingereza, hapa ikiwa ni katika kanisa kuu la St Paul's, London.
Moon, pictured large and reddish in tone, above Hull apartments in Yorkshire, UK

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Picha hii ilipigwa na mpiga picha Danny Lawson, mjini Hull, Uingereza