Saratani Kenya: Kikundi kimoja mjini Nairobi kimejitolea kuwashonea matiti ya kubandika

Maelezo ya video, Kikundi kimoja mjini Nairobi kimejitolea kuwashonea matiti akina mama waliokatwa matiti

Kikundi kimoja mjini Nairobi, Kenya kimejitolea kuwashonea matiti ya kubandika, akina mama waliokatwa matiti baada ya kuathiriwa na saratani ya matiti. Wanaziita Knockers.

Baadhi ya wanachama wa kikundi hiki ni wanawake wanaougua saratani ya matiti na wanaume ambao wake zao walifariki kutokana na saratani. Wanatumia nyuzi na pamba kuwapa waathiriwa chaguo mbadala, badala ya titi la silicone ambalo wengi wanasema ni zito, huteleza sana, ni bei ghali na wengi hukosa zile zinawatosha.

Video: Mercy Juma.